Mume Kichwa

MUME – KICHWA

Katika miaka hii yote nilikuwa na wazo kuwa mwanamume wa shoka halii. Lakini sikuwa nimezingatia kuwa Yesu mwenyewe alilia hadharani. Baada ya kujua, mawazo yale mafinyu yalianza kutoweka .
Umwanaume wa mtu haupimwi kwa kuvumilia kisabuni yaani kulia ndani kwa ndani, bali kupimwa kwa kukabiliana na matatizo bila hasira, vurugu na kujihami. Kutolia ni ubinasfi wa kuepusha aibu. Kudhibiti hasira, ndio hasa utawala wa kweli, na kutimiza majukumu yetu hasa katika kuwafanya wale wanaotuzunguka kujisikia kulindwa zaidi.
Mith 16:32 “Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji” Mith 16:32
Paulo anaeleza mafungu kadha wa kadha kuelezea mamlaka ya Mume katika familia.
“Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo; naye ni mwokozi wa mwilli” Efeso 5:3
“Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanaume ni Kristo, na kichwa cha mwanmke ni mwanaumume, na kichwa cha Kristo ni Mungu” 1 Wakor 11:3
Uongozi wa kweli
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili kuwa mmoja. Kwa hiyo hakuna namna yeyote mtu hawezi kujishinda mwenyewe. “Kwa kuwa kiungo kimoja kikiumia vyote vimeumia” 1 Kor 12:26
Neno la kiyunani lililotumika hapa kumaanisha kichwa ni Kephal lenye maana ya mtawala, kiongozi. Hivyo mwanamume ni mtawala wa mwanamke.
Lakini Mungu hutazamia nini kutoka kwa Wanaume?
“Msitende neno lolote, kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake” Wafilipi 2: 3
Wanaume mmezaliwa ili kuwa vichwa- kuwa kichwa cha mwanamke wa pekee, simama kutetea wito wako.


Mamlaka
Mamlaka ya mwanaume sio ubunifu wa mtume Paulo. Ni maamuzi ya Mungu mwenyewe, hili linafundishwa kwenye agano la kale na agano jipya. Hata katika Kitabu cha uUfunuo wa Yohana, kanisa la Mungu linafananishwa na Bibi arusi, ikielekeza uhusiano uliopo kati ya mwanaume na mwanamke ndio ule uhusiano wa Kristo na kanisa lake.
Hatuwezi kuepuka hili: Wanaume, Wababa wanayo mamlaka. Lakini tumekuwa na uelewa tofauti katika kuelewa mamlaka hayo. Akieleleza mamlaka hayo Yesu mwenyewe anasema
“Lakini Yesu akawaita akasema, mwajua ya kuwa wakuu wamataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakiwi hivyi kwenu, bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa, na awe mtumishi wenu, na mtu yeyote atakayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu” Matayo 20:25 – 28
Mamlaka yako yanavyokua ndivyo majukumu yako yanavyokuwa makubwa mbele za Mungu aliyekupa mamlaka hyo.
Mamlaka ni kuwajibika
“Enyi waume , wapendeni wake zenu, kama kristo naye alivyolipenda kanisa , akajitoa kwa ajili yake, ili kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wla kunyanzi wala lolote kama hayo;bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa wanaume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendae mkewe hujipenda mwenyewe…………………..” Efeso 5:25- 28
Neno la kiingereza lililotumika majukumu ni Responsibilty ina maana ya abilty to respond yaani uwezo wa kuitikia. Katika familia ni uwezo wa kukabiliana na majukuku ya msingi katika familia.
Katika upendo kuna uhuru, mwanamke wa Kikrsto hawezi kuwa mwanamke kielelezo kama hatapewa uhuru wa kutenda. Mume aliye kichwa atakuwa mwenye imani na mkewe. Ili mwanamke huyu awe mwanamke wa Mithali 31 lazima iwe kama neno linavyosema “Moyo wa Mumewe humwamini” uongozi na mamlaka ya kweli humwamini mke wake.
Mume mwenye mamlaka na uongozi wa kweli atamtia moyo mkewe na kukuza vipaji na talanta zake hata shughuli za kiuchuni zitaendelea. Kama mume waweza mara nyingine ukawa mtu wa kumlaumu mkeo kuwa amekosa sifa za mwanamke wa mithali 31. Lakini kama hutapalilia na kuona umuhimu wa mke wako huwezi kufikia tabia za mwanamke mwema.
Yesu alitoa kanuni rahisi ya ukubwa. Wakristo tunaongoza kwa kuwa mfano bora au kwa kutangulia kama Yesu alitoa mfano akatuachia kielelezo tufauate nyayo zake (1Petr 2:21)Ili kuwa kiongozi wa kweli katika familia lazima uongoze kwa kuwa ,fano wa kweli.

KIMWILI : Hakikisha unakuwa mtu wa kazi, kwa kutimiza amri ya Mungu ya nne Kutoka 20:8 …….. ….. siku sita fanya kazi……….. kama Kichwa cha familia fanya kazi sisitiza kufanya kazi kwa watu wa nyumbani mwako.
KIAKILI: Kama Kichwa cha familia onesha njia kwa kusoma, kujiendeleza , kusoma vitabu vya ujuzi mbalimbali. Ujuzi wa kiroho kwa kusoma Biblia na vitabu vyo roho ya unabii
KIROHO: Kama kichwa uwe mstari wa mbele kwa mambo ya kiroho, kuwahi kanisani , kuhimiza maombi nyumbani, utoaji wa zaka na sadaka na hata kuifanya kazi Bwana
KAMA BABA WEWE NI KUHANI ITISHA MAOMBI YA FAMILIA ASUBUHI NA JIONI
Tumeitwa kuwa vichwa, kuwa vichwa sio kugangamala bali ni ni kuwa kielelezo katika mmbarak wa familia Mungu aliotupatia. Hatuwezi kuwa vielelezo tu la isipokuwa tunapaswa kumuita Bwana aingie ndani ya maisha yetu ili tubadilike. Tunapokuwa tayari kwa mabadikliko Mungu naye atakuwa radhi kutubadilisha.
BWANA AWABARIKI SANA